Labels

Monday, 14 March 2022

SAFARI YA KUTAFUTA PESA.




Sehemu ya kwanza.

KWANINI PESA INATAFUTWA NA KILA MTU?

Majibu utayaona mwishoni.

Siku za nyuma enzi za shule nakumbuka shairi moja lilikuwa na kichwa kinaitwa KAMA MNATAKA MALI, MTAIPATA SHAMBANI.

Kilikuwa kisa kimoja cha Baba ambaye alikuwa anaumwa sana kiasi ambacho hakukuwa na matumaini yoyote ya kupona.

Watoto wake walikaa pembeni mwa kitanda cha mgonjwa wakaanza kumsumbua sana wakisema TUONESHE MALI ZITAKAZOTUSAIDIA SISI WANAO.

Mzee wa watu kama walivyo wazee wengi huwa wanamaliza safari yao ya duniani bila kufanya jambo lolote litakalokuwa msaada kwa WATOTO aliowazaa mwenyewe bila kulazimishwa.

Basi mzee akawa hana majibu ya kuwapa wale watoto kwa sababu alikuwa HANA MALI ZA KUWAACHIA ZAIDI YA KUWAPA WOSIA TU.

Basi, mzee wa watu ikabidi awambie watoto wake kwamba YEYE HAJAACHA PESA WALA DHAHABU.

Hivyo akawapa ujumbe mgumu sana kwamba hawataweza kutoboa kama watasubiri kustarehe kwa mali alizotafuta mzee.

Kauli ile ilikuwa ndani yake kuna sharti, alisema KAMA MNATAKA MALI, MTAIPATA SHAMBANI.

Watoto wale walilalamika kwamba akili zao ni nyembamba hazijui mafumbo, ila WAPI mzee hakubadilisha kauli yake.

Mwisho wa siku mzee akakata roho na hatimaye watoto wale wakabaki NJIAPANDA SEGEREA.

Wanajiuliza waende Gongolamboto, au warudi Kariakoo au wakunje kona.

(Nimechukulia kama wale watoto walikuwa DSM, Kingekuwa kizazaa)

Walipokaa na kutafakari kwa kina wakagundua kwamba mzee aliwapa jukumu la KUFANYA KAZI ILI WAWEZE KUISHI.

Ile stori iliyoimbwa kwa njia ya shairi ilikuwa ina visa vingi na mikasa mingi sana..

Lakini mwisho inaonesha kwamba wale watoto waliamua kutoa mikono mfukoni.

Walifanya kazi kwelikweli, wakapata mafanikio makubwa wakapandisha MAJENGO YA MAANA mpaka maisha yao yakawa bora kuzidi yale aliyowaachia mzee.

Katika safari ya kutafuta pesa tutaona mengi sana lakini zaidi ya yote ni muhimu kuweka kichwani jambo hili kwamba.. KAMA HUTAFANYA KAZI, BASI ITAKUWA VIGUMU SANA KUISHI MAISHA YA NDOTO ZAKO.

Najua unatamani kujifunza mengi katika safari hii...

Usibanduke endelea kufuatilia hatua kwa hatua mpaka tutaimaliza safari hii ukiwa mtu wa tofauti sana.

Mimi ndiye dereva wako mkuu katika safari hii... Niiite Festo Amos, au Coach Amos..naaaam kwa msaada wa Mungu tutafika salama

Lakini Ndugu zangu watanzania, Tufanye kazi kwa bidii kama alivyotusisitiza Hayati MAGUFULI.

Na kama alivyosema Mwl. JK NYERERE kwamba kazi ni uhai, basi tufanye kazi bila kuweka kisingizio chochote ili uchumi wa mtu mmoja mmoja uweze kukua na hatimaye taifa letu liinuke kiuchumi.

TUKIWA NA NGUVU YA PESA, TUTAISHI MAISHA MAKUBWA.

@Festo Amos
@Coach Amos.
0766181367.

#liveagreatlife
#nguvuyapesa.

No comments:

Post a Comment

SAFARI YA KUTAFUTA PESA.

Sehemu ya kwanza. KWANINI PESA INATAFUTWA NA KILA MTU? Majibu utayaona mwishoni. Siku za nyuma enzi za shule nakumbuka shairi moja lilikuwa ...